Chuo kikuu Al-Ameed kinaendesha opresheni ya kugawa chakula cha mwezi wa Ramadhani

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinaendesha opresheni ya kugawa chakula cha mwezi wa Ramadhani kwa familia za mafakiri na watu wenye kipato kitogo, chini ya walimu, watumishi na wanafunzi wa chuo hicho.

Katika mpango wa kusaidia familia hizo, hususan ndani ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, na kusaidia kupunguza ukali wa maisha katika kipindi hiki kigumu.

Kwa mujibu wa maelezo ya makamo rais wa chuo Dokta Alaa Mussawi kwa mtandao wa Alkafeel, amesema: “Kitengo cha maelekezo ya nafsi na muongozo wa malezi kimesimamia zowezi hilo, na imekuwa kawaida yake kufanya hivyo kila mwaka kwa ajili ya kutumikia raia wa taifa letu kipenzi, walimu wa chuo na wanafunzi wanajitolea kufanya kazi hiyo, sambamba na kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu, unao himiza umuhimu wa kusaidiana katika jamii, hasa kusaidia familia zenye maisha magumu katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani”.

Akaongeza kuwa: “Opresheni hii imehusisha nyumba kadhaa za mafakiri na watu wenye kipato kidogo katika mkoa wa Karbala, furushi la chakula lina aina nyingi za vyakula vinavyo hitajiwa na familia hizo katika mwezi huu mtukufu”.

Kumbuka kuwa chuo kikuu cha Al-Ameed kinafanya shughuli nyingi za kibinaadamu na kinatoa michango mbalimbali katika sekta hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: