Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kupitia tawi lake la Najafu, imeandaa nadwa ya Quráni iliyo ipa jina la (kisomo cha Imamu Hassan Almujtaba –a.s- kwa Abu Abdurahmani Sulami –r.a- matamshi na maelekezo), chini ya uhadhiri wa Dokta Muammal Jawadu Khalifah mmoja wa watafiti wa Quráni katika tawi hilo.
Nadwa imefunguliwa kwa Quráni tukufu iliyo somwa na Ali Muslim, baada ya ufunguzi huo mtoa mada akaeleza mtazamo wa kielimu kuhusu mapokezi ya kwamba Imamu Hassan (a.s), alisoma Quráni tukufu mbele ya Taabii Abu Abdurahman Sulami –r.a-, akatoa dalili za kielimu zilizo bainisha kuwa Imamu Hassan (a.s) ni mmoja wa Maimamu watakatifu ambao wako sawa na Quráni tukufu, naye ni miongoni mwa watu waliotajwa na Mtume kuwa wanaifahamu zaidi Quráni, akatoa ushahidi mwingi wa aya na hadithi za Mtume (s.a.w.w) pamoja na riwaya za Maimamu wa Ahlulbait (a.s).
Nadwa hiyo imehudhuriwa na kundi kubwa la waumini wakiwa wamechukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi, aidha kulikuwa na nafasi ya kutoa maoni na kuuliza maswali kwa waliokuwa ndani ya ukumbi na wale walioshiriki kupitia jukwaa la (Google Meet), maswali mengi yameulizwa na kujibiwa pamoja na michango mbalimbali imetolewa kutoka kwa washiriki.
Kumbuka kuwa nadwa hii ni moja ya harakati za Maahadi ya Quráni tukufu, chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu kupitia matawi yake tofauti, kwa ajili ya kueneza utamaduni wa kufanyia kazi mafundisho ya Quráni tukufu katika jamii.