Bora kushinda miezi elfu moja: Ibada za usiku wa Lailatul-Qadri wa pili

Maoni katika picha
Usiku wa mwezi ishirini na moja Ramadhani ni moja ya siku za Lailatul-Qadri, nayo ni bora kushinda usiku wa mwezi kumi na tisa, tambua kuwa usiku wa Lailatul-Qadri ni mmoja, bali kunatofauti ya kubaini siku husika, lakini hutarajiwa kupatikana katika moja ya siku hizi tatu (19 – 21 – 23).

Ibada za siku hizo zimegawanyika sehemu tatu:

Sehemu ya kwanza: Ibada zinazo patikana katika siku zote za Lailatul-Qadri, ambazo ni:

 • - Kuoga: bora uoge wakati linapo zama jua na uswali magharibaini ukiwa umesha oga.
 • - Kuswali rakaa mbili, katika kila rakaa baada ya kusoma Alhamdu, usome surat Tauhidi mara saba, na baada ya kutoa salamu usome mara sabini uradi huu (Astaghafirullaha wa atubu ilaihi).
 • - Kufungua msahafu mtukufu na kuushika mikononi mwako kisha unamuomba Mwenyezi Mungu kwa utukufu wa msahafu huo kwa kusema: (Ewe Mola mimi nakuomba kwa utukufu wa kitabu chako na yaliyomo ndani ya kitabu chako, limo jina lako tukufu… hadi mwisho wa dua kama ilivyo andikwa kwenye vitabu vya dua).
 • - Kuweka msahafu kichwani na kusema: (Ewe Mola kwa utukufu wa Quráni hii, na kwa utukufu wa aliye teremshiwa… hadi mwisho wa dua kama ilivyo andikwa katika vitabu vya dua).
 • - Kuzuru kaburi la Imamu Hussein (a.s), imepokewa katika hadithi kuwa: (Ikifika siku ya Lailatul-Qadri unatoka wito katika mbingu ya saba ndani ya Arshi usemao, Mwenyezi Mungu amemsamehe aliyezuru kaburi la Hussein –a.s-).
 • - Kuswali rakaa mia moja, hakika swala hiyo inafadhila nyingi, katika kila rakaa baada ya Alhamdu inapendeza kusoma surat Tauhidi mara kumi.
 • - Kusoma dua ya: (Ewe Mola mimi nimeshinda nikiwa mtumwa wako, similiki manufaa ya nafsi yangu wala madhara… hadi mwisho wa dua kama ilivyo andikwa katika vitabu vya dua).
 • - Kusoma dua ya Jausheni kubwa. Angalia katika kitabu cha Mafaatihul-Jinaani.

Sehemu ya pili: Ibada zinazo patikana katika siku zote kumi za mwisho:

Usiku wa mwezi ishirini na moja ni usiku wa kwanza katika siku kumi za mwisho, miongoni mwa ibada za kufanywa katika siku hizo ni:

 • - Uombe dua hii, nayo ni dua ya Imamu Swadiq (a.s) aliyo kuwa akiisoma katika kumi la mwisho: (Ewe Mola mimi najilinda kwa utukufu wako, usije ukaisha mwezi wa Ramadhani au ichomoze Alfajiri ya usiku huu nikiwa na dhambi au kosa la kusababisha uniadhibu).
 • - Usome dua iliyopokewa na Imamu Swadiq (a.s), aliyokuwa anaisoma kila siku katika kumi la mwisho isemayo: (Ewe Mola hakika wewe unasema katika kitabu chako ulicho teremsha… hadi mwisho wa dua kama ilivyo andikwa na vitabu vya dua).

Sehemu ya tatu: Ibada na dua maalum za usiku huu:

Dua maalum za usiku hii ni:

 1. Usome dua hii (Ewe unae ingiza usiku katika mchana, na unaingiza mchana katika usiku, unatoa uhai katika umauti, na umauti katika uhai… hadi mwisho wa dua kama ilivyo andikwa katika vitabu vya dua.
 2. Usome dua hii pia (Ewe Mola mtakie rehema Muhammad na Aali Muhammad, unipe elimu itakayo funga mlango wa ujinga, na uongofu utakao niepusha na kupotea, na utajiri utakao funga mlango wa ufakiri… hadi mwisho wa dua kama ilivyo andikwa katika vitabu vya dua).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: