Kumbukumbu ya kifo cha kiongozi wa waumini Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s)

Maoni katika picha
Tupo katika siku zenye msiba mkubwa baada ya msiba wa kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), nao ni msiba wa kifo cha pambo la Dini kiongozi wa waumini Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s), waziri wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na khalifa wake baada yake kwa walimwengu wote, aliye uwawa mwezi ishirini na moja Ramadhani mwaka wa arubaini hijiriyyah.

Riwaya zinaonyesha kuwa katika usiku wa mwezi ishirini na moja kiongozi wa waumini (a.s) alizimia kwa muda kisha akazinduka, akasema: Huyu hapa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) na Ammi yangu Hamza, na ndugu yangu Jafari, na maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), wanasema: Njoo haraka tumekukumbuka, kisha akazungusha macho yake kuwaangalia watu wa nyumbani kwake, halafu akasema: Nakuageni, Mwenyezi Mungu akupeni subira, Mwenyezi Mungu akulindeni, mtabaki na Mwenyezi Mungu naye atosha.

Kisha akasema: Wa alaikum salaam ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, kisha akasema: “Kwa mfano huu watende watendao… Hakika Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wachamungu na wanye kutenda wema” macho yake yakatoka machoji, akaendelea kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wingi na kutamka shahada mbili, halafu akaelekea kibla na akafumba macho na akanyoosha miguu na mikono, akasema: Nashuhudia kuwa hakuna Mungu ispokua Alla mmoja wa pekee asiyekua na mshirika, na ninashuhudia kuwa Muhammad ni mja wake na Mtume wake, kisha akafa (a.s) na roho ikaaga dunia.

Ewe Imamu!! Ewe Ali!! Ewe bwana wetu..

Sauti za vilio zikawa nyingi.. watu wa mji wa Kufa wakatambua kuwa kiongozi wa waumini (a.s) amefariki, wakaja kwa wingi wanawake na wanaume, wakamiminika makundi kwa makundi, vilio vikaenea mji mzima wa Kufa, ikaenea huzuni kubwa mji wote kama siku aliyokufa Mtume (s.a.w.w).

Muhammad bun Hanafiyya anasema: Ulipofika usiku wa mwezi ishirini na moja, baba alikusanya watoto wake na watu wa nyumbani kwake akawahesabu mmoja mmoja, kisha akasema: Mwenyezi Mungu ndio khalifa wangu kwenu, naye anatosha na ndio mbora wa kutegemewa.

Sumu ilikuwa imeenea katika muili wake, nyayo zake zilikuwa nyekundu kutokana na sumu, jambo hilo lilituumiza sana na kutukatisha tamaa, tukampa chakula na maji hakuweza kula wala kunywa, akaendelea kumtaja Mwenyezi Mungu, halafu akawaita watoto wake wote kwa majina yao, akaanza kuwaaga huku wanalia, Hassan akasema: kwa nini unafanya hivi? Kiongozi wa waumini (a.s) akasema: Ewe mwanangu nimemuona babu yako Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) katika usingizi, nikamshtakia hali niliyo nayo na maudhi ninayo pata katika umma huu, akaniambia: omba kwa Mwenyezi Mungu. Nikasema: Ewe Mola wabadilishie shari kuliko mimi, na unibadilishie kheri kuliko wao, Mtume akasema: Mwenyezi Mungu amekubali dua yako, utakuja kwetu baada ya siku tatu, na tayali siku tatu zimeisha, ewe baba Muhammad na ewe baba Abdullahi nawausia kheri, nyie mnatokana na mimi na mimi natokana na nyie.

Kisha akageukia watoto wake wengine, akawausia wasitengane na ndugu zao watoto wa Fatuma (a.s) yaani Hassan na Hussein (a.s), kisha akasema: Mwenyezi Mungu akupeni maombolezo mema, tambueni mimi naondoka katika usiku huu, nitakutana na kipenzi wangu Muhammad (s.a.w.w) kama alivyo niahidi, akamuambia mwanae Hassan: Nikifa nioshe na univishe sanda halafu uniweke marashi yaliyo baki katika marashi ya babu yako Mtume wa Mwenyezi Mungu, hakika yanatokana na kafuur ya peponi, aliletewa na Jibrilu, kisha niweke kwenye kitanda (jeneza), wala asitangulie yeyote mbele ya kitanda (jeneza) wakati wa kwenda kunizika, bebeni kwa nyuma na mfuate kitakako elekea, kitakapo wekwa sehemu yake ya mbele basi na nyie wekeni hapo ndio mahala pa kaburi langu, kisha wewe Abu Muhammad upite mbele na kuniswaliya upige takbira mara saba…
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: