Shirika la Nuurul-Kafeel linafafanua sababu ya kuongezeka bei kwa baadhi ya bidhaa zake

Maoni katika picha
Shirika la Nuurul-Kafeel linalo tengeneza bidhaa za vyakula limetaja sababu ya kuongezeka bei ya baadhi ya bidhaa zake katika siku za hivi karibuni kutokana na mambo yaliyo nje ya uwezo wa shirika.

Shirika limesema kuwa: Miongoni mwa sababu zilizo sababisha ongezeko hilo la bei ni:

  • - Kushuka kwa thamani ya Dinari mbele ya Dola katika vitu vinavyo agizwa nnje pamoja na bidhaa za ndani ambazo zinategemea malighafi kutoka nje, jambo ambalo limepelekea kuongezeka bei yake kwa Dinari.
  • - Uchache wa malighafi za ndani umesababisha kupanda kwa thamani ya malighafi na kusababisha kupanda bei ya bidhaa zinazo tengenezwa hapa nchini.
  • - Kuhusu bei ya kuku hai katika soko na kuku wetu wa ndani, asilimia %25 ya uzani wa kuku sokoni hupotea kwa (kutoa kichwa, miguu, manyoya na utumbo), bei ya kuku baada ya kutoa vitu hivyo huwa rahisi kitogo ukilinganisha na wale wanao agizwa kutoka nje ya nchi, tumeangalia namna ya kulinda wazalishaji wa ndani, huchinjwa chini ya usimamizi wa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kuhakikisha uhalali na ubora.

Shirika limemaliza kwa kusema: Bila shaka shirika la Nuurul-Kafeel toka lilipo anzishwa limekua likijitahidi kuzalisha bidhaa halali zenye ubora mkubwa kwa bei nafuu anayo weza kuimudu kila mwananchi wa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: