Kikosi cha chuo cha Maarifa ya elimu za kiislamu kimepata nafasi ya kwanza katika shindano la (maarifa ya turathi)

Maoni katika picha
Kikosi cha chuo cha maarifa ya elimu za kiislamu kimepata nafasi ya kwanza katika shindano la (maarifa ya turathi), lililosimamiwa na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, baada ya kukishinda kikosi cha chuo kikuu cha Ahlulbait (a.s) katika raundi ya mwisho.

Makundi hayo mawili yamefanya raundi zao za mashindano ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, mbele ya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Abdulhussein Ashiqar na kundi la viongozi wa Ataba.

Kikosi cha chuo cha maarifa ya kiislamu kimekishinda kikosi cha chuo kikuu cha Ahlulbait (a.s) kwa alama (20 – 70) kwa raundi tatu, waliulizwa maswali tofauti katika mazingira ambayo hakuna msaada, na mazingira ya ushindani yalikua makubwa.

Kikosi cha maarifa ya elimu za kiislamu kikapata nafasi ya kwanza yenye zawadi ya kwenda Umra, na washindi wa pili ambao ni kikosi cha chuo kikuu cha Ahlulbait (a.s), wakashinda zawadi ya kwenda kumzuru Imamu Ridhwa (a.s).

Tambua kuwa shindano la (maarifa ya turathi) linahusisha vikundi vya turathi katika mwezi wa Ramadhani na limefanywa kwa mara ya kwanza na kurushwa moja kwa moja kwenye luninga mbalimbali za Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: