Kuendelea kwa vikao vya usomaji wa Quráni ndani ya mwezi wa Ramadhani katika mkoa wa Baabil

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Baabil chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu linaendesha vikao vya usomaji wa Quráni katika wilaya ya Mahawil, sambamba na kuomboleza kifo cha kiongozi wa waumini Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s) na kwa ushiriki wa jopo la wasomaji wa Maahadi katika mkoa huo, sambamba na kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi.

Mahafali ya kikao cha usomaji wa Quráni kimepambwa na visomo vya wasomaji wawili ambao ni Saahir Tamimi na Sayyid Ahmadi Aáraji, ukafuata muhadhara wa Dokta Sayyid Haidari Shallaah, aliyebainisha utukufu wa kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s) na historia ya uhai wake, pamoja na mchango wake katika kusambaza uislamu duniani.

Hafla ikahitimishwa kwa kaswida na mashairi yaliyo husu kifo cha Imamu Ali (a.s) chini ya uimbaji wa Ahmadi Silawi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: