Mawakibu Husseiniyya zinagawa futari katika mji wa Karbala

Maoni katika picha
Mawakibu Husseiniyya zimeanza kugawa futari kwa watu wanaokuja kuzuru malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), toka siku za kwanza katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Huduma hiyo huongezeka katika siku za Ijumaa, ambapo ukarimu, mapenzi na undugu huonekana wazi kwa wakazi wa mji huu mtakatifu, pamoja na mawakibu na vikundi vya Husseiniyya vinavyo kuja kutoka nje ya mji.

Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili takatifu Husseiniyya na Abbasiyya, bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Katika mwezi mtukufu wa Ramadhani mawakibu za kutoa huduma hupika chakula na kugawa futari kwa mazuwaru, katika barabara na njia zinazo tumiwa na mazuwaru kwa wingi, hupanga aina tofauti za vyakula kwenye barabara hizo karibu na muda wa futari, utawaona wanashindana katika kuwahudumia mazuwaru waliofunga, kama wanavyo shindana wakati wa kuhudumia mazuwaru kwenye ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu Muharam na Arubaini”.

Akaongeza kuwa: “Kazi za mawakibu hizo hufanywa chini ya utaratibu ambao hukubaliana viongozi wa mawakibu, huteua sehemu za kupanga chakula kwa namna ambayo haziathiri harakati za mazuwaru wala hazisababishi msongamano”.

Kumbuka kuwa huduma hii ni muendelezo wa huduma ambazo hutolewa na mawakibu hizo wakati wa msimu wa huzuni katika mwezi wa Muharam na Safar, pamoja na kwenye matukio mengine ndani ya kipindi chote cha mwaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: