Chuo kikuu cha Alkafeel kimetengeneza anuani mpya ya toghuti yake

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetengeneza anuani mpya ya toghuti yake ambayo ni: (http://alkafeel.edu.iq).

Rais wa chuo Dokta Nuris Muhammad Shahid Dahani amesema kuwa: “Hakika toghuti hii imesaidia utoaji wa huduma kwa njia ya mtandao, ni nyepesi katika utendaji wake na rahisi kutumiwa na wanafunzi pamoja na wakufunzi”.

Akasisitiza kuwa: “Kutengeneza anuani mpya ya Toghuti kumeifanya kuwa na muonekano mpya wa kupendeza, sambamba na kuboresha hutuma zake tofauti, kazi hiyo imefanywa na watumishi wetu wa kitengo cha teknolojia na taaluma, kwa kushirikiana na kituo cha ufundi na taaluma Alkafeel”.

Makamo rais wa chuo Dokta Nawaal Almayali amesema: “Anuani mpya inakinga imara inayo endana na mifumo inayo tumika duniani kwa sasa”.

Akafafanua kuwa: “Toghuti mpya inauwezo wa kuongeza huduma mpya katika kurasa maalum, kwa mfano habari, matangazo na mikutano ya kimataifa pamoja na semina na harakati mbalimbali”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: