Shindano la Ramadhani kwa vijana wa Alkafeel: 28 Ramadhani ndio mwisho wa kupokea majibu

Maoni katika picha
Kamati inayo simamia shindano la kijana wa Alkafeel linalo fanyika kwa njia ya mtandao katika mwezi wa Ramadhani, linalo husu wanafunzi wa vyuo vikuu na shule za Iraq, imetangaza kuwa inaendelea kupokea majibu ya maswali yaliyo ulizwa kwenye shindano hilo, hadi sasa kunazaidi ya washiriki (3000), bado kamati inaendelea kupokea majibu hadi tarehe (28) Ramadhani.

Shindano linafanywa kwa mwaka wa pili mfululizo na kamati ya mahusiano ya vyuo vikuu na shule zilizo chini ya kitengo cha uhusiani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ikiwa ni miongoni mwa harakadi za mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel.

Mjumbe wa kamati inayo simamia shindano hili na kiongozi wa ofisi ya harakati za vyuo katika idara hiyo Ustadh Muntadhwiru Swafi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Shindano la awamu hii limepata mwitikio mkubwa kutoka kwa wanafunzi wa vyuo na Maahadi mbalimbali pamoja na wanafunzi wa shule za sekondari (upili), muitikio huu unatokana na mapenzi ya kushindana kwa kundi hili na kutaka kutabaruku na zawadi zinazo tolewa kwa washindi”.

Akaongeza kuwa: “Tarehe ya mwisho ya kupokea majibu ni (28) Ramadhani, matokeo yatatangazwa usiku wa kuamkia Idil-Fitri, watachaguliwa washindi (30) baada ya kupigia kura majibu sahihi, watapewa zawadi maalum pamoja na zawadi nyingine watakayo pewa washiriki wote”.

Katika kuhitimisha maelezo yake akasisitiza kuwa: “Tumia link ifuatayo kushiriki kwenye shindano hili: (https://alkafeel.net/cont) baada ya kufungua link hiyo jaza fomu maalum ya ushiriki, ukipata changamoto yeyote unaweza kuwasiliana nasi”.

Kumbuka kuwa shindano hili ni moja ya harakati zinazo fanywa na idara, linalenga kuongeza kiwango cha elimu na utamaduni kwa washiriki, kupitia majibu yao ya maswali yanayo ulizwa kwenye shindano, yanayo lenga kunufaika na mwezi huu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: