Mgahawa wa nje unagawa futari kila siku kwa mazuwaru

Maoni katika picha
Mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa nje uliopo katika barabara ya (Najafu / Karbala) unagawa futari kila siku kwa watu wanaokuja kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kufuata masharti ya afya.

Kiongozi wa mgahawa huo Sayyid Kaadhim Twahir ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tunagawa futari kila siku ndani ya mwezi wa Ramadhani, kiwango cha ugawaji wa futari huongezeka katika usiku wa Ijumaa na Lailatul-Qadri, kwani siku hizo huwa na watu wengi wanaokuja kutembelea malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), ukizingatia kuwa barabara ya (Najafu / Karbala) ni miongoni mwa njia kuu zinazo elekea katika malalo hizo takatifu, mgahawa ni sehemu ya kituo cha kuhudumia mazuwaru katika mwezi wa Ramadhani, huandaa futari kwa ajili ya mazuwaru kila siku”.

Akaongeza kuwa: “Milango ya mgahawa iko wazi kila siku ikiwa ni pamoja na ndani ya mwezi wa Ramadhani, huwa tunaandaa futari kwa ajili ya mazuwaru pamoja na matunda, maji, juisi na maziwa, huduma hizo ni sehemu ya ratiba maalum ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika mwezi huu, shughuli zote kuanzia kupika hadi kugawa chakula zinazingatia kanuni za kujikinga na maambukizi, kwa ajili ya kulinda usalama wa mazuwaru na watoa huduma”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalum ya mwezi wa Ramadhani, yenye vipengele vingi, kikiwemo hiki ambacho hufanywa kila mwaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: