Muonekano wa nuru katika malalo: minara ya malalo ya Abulfadhil Abba+si (a.s)

Maoni katika picha
Pembezoni mwa kubba takatifu la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) inaonekana minara miwili, kila mnara unangazi ambayo hutumika kuingia ndani yake kutokea tabaka la chini la haram tukufu, hadi kwenye kibalaza cha mnara kilichopo katika nusu ya juu ya mnara.

Kibaraza kinasehemu mbili zilizo tengenezwa kwa umaridadi mkubwa, sehemu ya juu ambayo inabaraza lenye mnara ni ya duara, ndefu na nzuri lakini duara lake ni dogo, mzunguko wake ni mt2.7 juu yake kuna taji dogo lenye matundu, na juu yake kumetengenezwa kwa madini yenye ujazo tofauti.

Nusu ya minara miwili ya juu imewekwa vifuniko vya madini, nusu ya chini imewekwa madini ya dhahabu yaliyotiwa mina, pamoja na kuzingatia umbo la mnara wa zamani na nakshi zake, zilizo wekwa hapa Iraq –wakati huo- ulikua mradi wa kwanza kufanywa na raia wa Iraq, chini ya kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, bila kutegemea msaada wowote kutoka nje, ulizinduliwa (4 Shabani 1431h) katika maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwenye malalo hii takatifu Abulfadhil Abbasi (a.s), hafla iliyo hudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Iraq.

Mzunguko wa mnara mmoja unaukubwa wa (mt11.85) na mzunguko wa (mt3.65), sehemu ya shina lake inauzunguko wa (mt13.18), urefu wake kuanzia chini ya haram ni (mt38.5) takriban, urefu wake wote kwa ujumla ni (mt44) takriban.

Minara imezungushiwa neno lisemalo (Yaa Hussein), pia kuna maneno mengine kama (Allah, Muhammad, Ali) na (Yaa Allah, Yaa Muhammad) na (Muhammad Rasulu-Llah, Ali Waliyyu-Llah).

Kiwango cha madini yaliyotumika katika minara miwili ni tani (12), vifuniko vya dhahabu vilivyo wekwa kwenye minara vimetengenezwa kwa kilo (108) ya dhahabu halisi iliyo wekwa kwenye ngozi ya mbuzi.

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu baada ya kumaliza ukarabati wa minara na uwekaji dhahabu uliofanywa na watumishi wake wa kitengo cha uhandisi, umezingatia kuhifadhi herufi zilizopo na zilirudiwa kuandikwa upya kwa kufuata vipimo vya kihandisi, na kuwekwa dhahabu iliyotiwa mina, tofauti itaendelea kuwepo kati ya minara ya malalo ya Imamu Hussein (a.s) na malalo ya mbeba bendera Abulfadhil Abbasi (a.s), ikiwepo tofauti ya kudumu ya mazingatio ya kiroho isiyo jificha kwa yeyote mwenye kutafakari, kuendelea kuwepo tofauti hiyo ni muhimu kwa kila mtu anayekuja kufanya ziara katika Ataba mbili takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: