Maahadi ya Quráni tukufu inawatahini zaidi ya mahafidh (60)

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Najafu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imewapa jaribio la awali mahafidh watakao shiriki kwenye shindano la kuhifadhi Quráni litakalo fanyika kwa mwaka wa tatu, jumla ya mahafidh (60) wameshiriki.

Jaribio hilo ni sehemu ya kuwapima wanafunzi watakao shiriki kwenye shindano hilo, litakalo fanywa katika tawi la Maahadi, mahafidh watakao fanya vizuri kwenye jaribio hilo watachaguliwa kushiriki kwenye shindano, linalo tarajiwa kufanywa mwezi (24) Ramadhani.

Kumbuka kuwa hili ni moja ya mashindano mengi yanayo simamiwa na Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, kwenye matawi yake tofauti, kwa ajili ya kusambaza utamaduni wa kufanyia kazi mafundisho ya Quráni tukufu katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: