Mawakibu za Waasit zinasaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo

Maoni katika picha
Wawakilishi wa mawakibu za mkoa wa Waasit chini ya kitengo cha Mawakibu na vikundi vya Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, wanagawa vifurushi vya chakula cha mwezi wa Ramadhani kwa familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo pamoja na mayatima, kwa ajili ya kusaidia kupunguza ukali wa maisha yao katika kipindi hiki kigumu.

Kiongozi wa wawakilishi hao bwana Daakhil Aniid Quraishi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mawakibu hutoa misaada katika kipindi chote cha mwaka, misaada yao sio ya msimu, na mwezi wa Ramadhani unaumaalum wake, huwa tunaongeza misaada na kusimama pamoja na familia za mafakiri na kujaribu kupunguza ukali wa maisha yao, tumeandaa ratiba kamili ya utoaji wa misaada hiyo, asilimia kubwa za mawakibu zinashiriki kwenye ratiba hiyo kugawa vitu vinavyo tolewa na watumishi wake”.

Akabainisha kuwa: “Vifurushi wanavyo gawa vina aina tofauti za vyakula, kunachakula kikavu na kilicho pikwa, nacho ni kile kinacho hitajiwa na familia katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, na kinacho saidia japo kidogo kupunguza makali ya maisha ya familia hizo katika kipindi hiki kigumu, hakika misaada tunayo toa ni kidogo ukilinganisha na ukubwa wa mahitaji ya familia hizo, tunawashukuru kwa kutukubalia japo hicho kidogo, na tunamuomba Mwenyezi Mungu pia atukubalie na atuondelee janga la virusi vya Korona katika taifa letu”.

Kumbuka kuwa rais wa kitengo cha Mawakibu na vikundi vya Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan, alisema kuwa: “Toka mwezi mtukufu wa Ramadhani ulipoingia Mawakibu Husseiniyya zimekua zikitoa misaada kupitia wawakilishi wake waliopo kwenye mikoa tofauti, wanagawa vifurushi vya chakula cha mwezi wa Ramadhani kwa familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo, chini ya ratiba maalum inayo jumuisha idadi kubwa ya wahitaji katika maeneo yaliyo pangwa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: