Mgonjwa wa zaidi ya miaka sitini amerudishiwa uwezo wa kusimama baada ya upasuaji

Maoni katika picha
Jopo la madaktari wa hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, limetangaza kufanikiwa katika upasuaji wa kurekebisha uti wa mgongo wa mgonjwa mwenye umri wa miaka sitini.

Daktari bingwa wa upasuaji katika hospitali hiyo raia wa Lebanon Dokta Aamir Sabáli amesema kuwa: “Hakika jopo la madaktari limefanikiwa kurekebisha pingili za uti wa mgongo wa mgonjwa mwenye umri wa miaka (63)”.

Akabainisha kuwa: “Mgonjwa alikua na tatizo kwenye pingili za mgongo lililokuwa limefikia asilimia (%35), alikuwa anapata maumivu makali na hakuwa anaweza kufanya shughuli za kawaida katika maisha”.

Akaendelea kusema: “Upasuaji umefanyika kwa muda wa saa tano chini ya madaktari bingwa wenye uzowefu mkubwa, pamoja na vifaa vya kisasa vilivyo tuwezesha kufanya upasuaji huo”.

Akasema kuwa: “Upasuaji umefanikiwa na mgonjwa anaendelea vizuri”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel inafanya juhudi daima za kutoa huduma bora kwa kutumia vifaa vya kisasa chini ya madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi, jambo ambalo limeifanya itoe ushindani mkubwa kwa hospitali za kimataifa duniani.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa waliobobea katika fani tofauti kila baada ya muda, sambamba na kupokea wagonjwa mbalimbali waliopo katika hali tofauti za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: