Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa kituo hicho Ustadh Bashiru Taajir, akaongeza kuwa: Masafa inayo tumika tangu siku ya kwanza ya mwezi wa Ramadhani inapatikana kwa anuani zifuatazo:
Satellite: Eutelsat 7A at 7.0 East(W3A)
DOWNLINK:12680.200 H
MOD:DVBS2
QPSK
FEC:5/6
Sr :3250
HD/MPEG-4
Akabainisha kuwa: “Ratiba ya matangazo hayo ipo kama ifuatavyo:
- - Swala ya Adhuhuri kwa mujibu wa nyakati za Karbala.
- - Usomaji wa Quráni kuanzia saa (11:00) hadi saa (12:00) Alasiri.
- - Swala ya Magharibi kwa mujibu wa nyakati za Karbala.
- - Dua Iftitaahi kuanzia saa (2:00) usiku.
- - Mawaidha yatatolewa na Shekh Abduswahibu Twaiy katika ukumbi wa Aljuud, kuanzia saa (4:00) hadi saa (5:00) usiku.
- - Mashindano ya usomaji wa Quráni kwa vikundi kuanzia saa (5:00) hadi saa (6:00) usiku.
- - Ratiba ya (Yaa Kaashiful-Kurbi) kwa lugha ya kiarabu –kila siku ya Alkhamisi- usiku wa Ijumaa saa (8:00) hadi saa (9:00) asubuhi.
- - Swala ya Alfajiri kwa mujibu wa nyakati za Karbala”.
Kumbuka kuwa kituo cha uzalishaji wa vipindi Alkafeel katika kila msimu wa kiibada ukiwemo mwezi wa Ramadhani, hutengeneza masafa ya bure yenye ubora mkubwa kwa ajili ya vituo vya luninga, huduma hii inanufaisha makumi ya vituo vya habari ndani na nje ya Iraq.