Vikundi vya Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Baabil chini ya Atabatu Abbasiyya, vimepata nafasi za juu katika shindano la Quráni lililofanyika katika siku za Lailatul-Qadri, ambapo kulikua na kikundi cha usomaji, kuhifadhi na tafsiri, shindano hilo liliandaliwa na kitengo cha masomo ya Quráni katika Maqaam ya Radi-Shamsi ya kiongozi wa waumini (a.s) kwa kushirikiana na taasisi za Quráni hapa mkoani.
Vikundi vilivyo wakilisha Maahadi na kupata nafasi tatu za kwanza ni: (Anasi Ibrahim Khaliil, Ali Qassim Rahiim, Ahmadi Hassan Hamza) katika usomaji, na (Ali Haadi Ali, Ali Makiy Abdul-Amiir, Ahmadi Haidari Swalehe) katika kuhifadhi.
Kumbuka kuwa tawi la Maahadi ya Quráni tukufu katika mkoa wa Baabil, linafanya harakati mbalimbali zinazohusu Quráni, pamoja na kutoa semina za Quráni mfululizo hapa mkoani.