Maahadi ya Quráni tukufu imefanya mashindano ya Quráni upande wa wanawake kwa awamu ya tatu

Maoni katika picha
Jumapili ya jana limefanywa shindano la kuhifadhi Quráni kwa wanawake awamu ya tatu, chini ya usimamizi wa tawi la Quráni tukufu la Najafu, jumla ya wanafunzi wa kike thelathini wameshiriki kwenye shindano halo.

Shindano limefunguliwa kwa Quráni iliyosomwa na Himam Tufaili, kisha Shindano likaanza ndani ya ukumbi wa jengo la tawi hilo, na kuhudhuriwa na wasomi wa Quráni pamoja na wazazi wa wanafunzi na walimu wa kituo cha Quráni tukufu cha Atabatu Alawiyya takatifu.

Shindano lilikuwa na sehemu tofauti, kulikuwa na maswali ya kidini pamoja na usomaji wa Quráni, sambamba na maswali ya hifdhu, chini ya jopo la majaji makini, na mwisho wa shindano hilo yakatangazwa majina ya washindi, kama ifuatavyo:

Kwanza: washindi katika waliohifadhi juzuu tano:

  • - Mshindi wa kwanza: Mahadi Muntadhiru Abdul-Huru.
  • - Mshindi wa pili: Kaadhim Jawaad Khuz-Ali.
  • - Mshindi wa tatu: Mustwafa Ali Adnani.

Pili: washindi katika waliohifadhi juzuu kumi:

  • - Mshindi wa kwanza: Ali Hashim Ibrahim.
  • - Mshindi wa pili: Ali Aadil Muhammad.
  • - Mshindi wa tatu: Mahadi Hamiid Msafiri.

Tatu: washindi katika waliohifadhi juzuu ishirini:

  • - Mshindi wa kwanza: Amjad Qassim Ali.
  • - Mshindi wa pili: Hassan Ali Takliif.
  • - Mshindi wa tatu: Muhammad Haadi Hisham.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: