Maoni katika picha
Maneno hayo yamesomwa na wasomaji wa Ataba hizo takatifu Husseiniyya na Abbasiyya, tunatarajia Mwenyezi Mungu amjalie kila muumini aweze kuufikia tena mwezi huu mwaka kesho, mazingira halisi yanasema: jua la mwezi mtukufu wa Ramadhani linaondoka na kuelekea kuzama, saa zake na siku zake zimeisha, tunauaga huenda ndio mara ya mwisho, na huenda tukakutana mwakani, kama Mwenyezi Mungu akitupa nafasi hiyo, hakika ni mgeni asiyekua na muda mrefu bali ni siku za kuhesabika, hakika zimeisha haraka.
Kuuaga mwezi mtukufu wa Ramadhani huanza siku tatu za mwisho katika mwezi huo, ni utamaduni wa kila mwaka ambao hufanywa na Ataba mbili tukufu, husomwa kaswida kwa Sauti nzuri zinazo ingiza hisia ya huzuni kwa msikilizaji katika kuuaga mwezi wa Mwenyezi Mungu, miongoni mwa maneno yaliyokua yanaimbwa na kusikika katika minara ya malalo mbili ni:
Kwaheri kwaheri.. ewe mwezi wa Ramadhani
Kwaheri kwaheri.. ewe mwezi wa kusimama
Kwaheri kwaheri.. ewe mwezi wa twaa na msamaha
Kwaheri kwaheri.. ewe mwezi wa wema na ihsani