Ofisi ya Marjaa Dini mkuu inatarajia kuonekana mwezi muandamo wa Idulfitri siku…

Maoni katika picha
Ofisi ya Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Ayatullahi Sayyid Sistani katika mji wa Najafu imesema kuwa, inatarajiwa kuwa mwezi muandamo wa Shawwal utaonekana kwa macho moja kwa moja siku ya Alkhamisi, hivyo Ijumaa itakuwa sikukuu ya kwanza ya Idulfitri.

Imeandikwa katika kurasa ya nyakazi za miezi miandamo inayo andikwa na ofisi hiyo kuwa, mwezi muandamo wa Shawwal unatarajiwa kuonekana jioni ya Alkhamisi mwezi (30 Ramadhani 1442h) sawa na tarehe (13 Mei 2021m) katika mji mtukufu wa Najafu wakati wa kuzama jua saa 12:51 jioni, kama ifuatavyo:

  • - Umri wake utakua saa moja na dakika 44 hadi 47.
  • - Urefu wake katika anga ni daraja 17 dakika 23.
  • - Muda wa kubaki angani baada ya jua kuzama ni saa 1 na dakika 33.
  • - Kiwango cha miale ya nuru ni %2,39.

Katika mazingira hayo utaonekana wazi ukiwa juu.

Pia unatarajiwa kuonekana jioni ya Jumatano mwezi (29 Ramadhani 1442h) sawa na tarehe (12 Mei 2021m) saa 12:50 jioni, kama ifuatavyo:

  • - Umri wake utakua saa moja na dakika 20 hadi 47.
  • - Urefu wake katika anga ni daraja 6 na dakika 59.
  • - Muda wa kubaki angani baada ya jua kuzama ni dakika 38.
  • - Kiwango cha miale ya nuru ni %0,52.

Katika mazingira hayo hautarajiwi kuonekana kwa macho.

Kumbuka kuwa: “Taarifa hii haiwakilishi rai ya Marjaa Dini, bali ni matarajio ya kianga (falaki), kwa sababu mwanzo wa mwezi hutegemea kuonekana kwa mwezi muandamo kisheria, kwa hiyo tunatarajia kwa waislamu wote waangalie mwezi kwa kuzingatia tamko hili, kama wakiuona watupe taarifa, wala wasitusahau katika dua zao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: