Ofisi ya Marjaa Dini mkuu leo siku ya Jumatano (29 Ramadhani 1442h) sawa na tarehe (12 Mei 2021m), imetoa tamko kuhusu mashambulio yanayo endelea Palestina.
Ifuatayo ni nakala ya tamko lililo andikwa katika toghuti ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Ayatullah Sayyid Sistani:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu
Marjaa Dini mkuu kwa mara nyingine anasisitiza kuwa pamoja na raia wa Palestina katika mapambano yao dhidi ya wavamizi wanao endelea kupora ardhi yao na kuchukua maeneo mengine ya Qudsi tukufu, tunatoa wito kwa kila mtu huru kuwasaidia kurudisha haki yao waliyo nyan’ganywa.
Hakika mapambano yanayo shuhudiwa katika viwanja vya Masjidi Aqswa na maeneo mengine siku hizi, yanaonyesha msimamo wa wapalestina katika kupambana na wavamizi waovu na jinai zao endelevu, na kutokuwa tayali kuachia ardhi yao iliyo vamiwa hata kama itawagharimu.