Zakatul-Fitri: kiwango chake.. nani apewe.. kwa mujibu wa Marjaa Dini mkuu

Maoni katika picha
Ofisi ya Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani imetaja kiwango za Zakatul-Fitri mwaka huu kuwa ni dinari elfu moja na mia tano (1500) kama mbadala wa unga.

Kiwango cha Zakatul-Fitri ni pishi, ambalo ni sawa na kilo tatu za ngano (unga), shairi, zabibu, mchele, tende na vinginevyo miongoni mwa vyakula vinavyo pendwa na watu wa eneo husika, au kutoa kiasi cha pesa kinacho lingana na thamani ya vyakula hivyo, ni wazi kuwa thamani yake inatofautiana kutokana na kutofautiana kwa miji, hivyo unapaswa kujua thamani ya kilo moja ya aina ya nafaka unayokusudia kutoa kabla haujatoa.

Zakatul-Fitri hupewa mafakiri na masikini ambao ni halali pia kupewa Zaka ya mali, tambua kuwa sio halali Zakatul-Fitri kupewa Hashimiyya inapokua imetoka kwa asiyekua Hashimiyya, wala haifai kumpa yule ambaye unawajibika kumhudumia kisheria kama baba, mama, mke na mtoto.

Masharti ya kuwajibikiwa na Zakatul-Fitri:

  • 1-
  • 2- Akili na kutozimia.
  • 3- Utajiri, nao ni kinyume cha ufakiri.

Mtu akikamilisha masharti haya kabla ya kuzama jua la siku ya mwisho ya mwezi wa Ramadhani hadi mwanzo wa usiku wa Idilfitri, atawajibikiwa kulipa Zakatul-Fitri yake na ya wanao mtegemea, sawa wawe ni wale ambao anawajibika kuwahudumia kisheria na wengine, wakati bora wa kutoa ni baada ya kuandama mwezi hadi kabla ya jua kugeuka katika siku ya Iddi.

Tambua kuwa pesa halisi sio Zakatul-Fitri, kwa sababu hakuna Zakatul-Fitri ya pesa, bali pesa ni badala ya pishi (kilo 3) za chakula, kwa hiyo ni lazima kuzingatia nia katika utoaji wa Zakatul-Fitri unapokua unatoa pesa, ujue kua unatoa pesa badala ya pishi la chakula.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: