Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake inafanya nadwa kuhusu tukio la Israa na Miraji

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya nadwa yenye anuani isemayo: (Safari ya Israa na Miraji katika mtazamo wa Quráni).

Kiongozi wa habari katika Maahadi hiyo Dokta Israa Akarawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Maahadi inafanya harakati tofauti katika mwezi wa Ramadhani, miongoni mwa harakati hizo ni kuadhimisha safari ya Mtume (s.a.w.w) kutoka Masjid Haraam hadi Masjid Aqswa na kwenda mbinguni”.

Akaongeza kuwa: “Teknolojia za kisasa zimetuwezesha kutoa vikwazo vya mawasiliano kila mahala, hivyo msemaji wa nadwa hii alikuwa ni Dokta Mawahibu Khatwibu kutoka chuo kikuu cha Almustwafa katika mji wa Qum, amezungumza mambo mbalimbali na kauli za wanachuoni na wafasiri”.

Akaendelea kusema: “Nadwa imepambwa na maswali pamoja na maoni kutoka kwa washiriki, mjadala wa kielimu ulikua mkubwa, uliofungua milango mipya ya maarifa, nadwa hii inalenga kueneza utamaduni wa kufanyia kazi mafundisho ya Quráni tukufu katika jamii ya wanawake”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tawi la wanawake inajukumu la kusambaza elimu kwa wanawake, ikiwa ni pamoja na “maarifa ya Quráni”, na kutengeneza kizazi cha wanawake wenye uwezo wa kufanya tafiti za kielimu katika kila sekta ya Quráni tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: