Jioni ya Alkhamisi (30 Ramadhani 1442h) sawa na tarehe (13 Mei 2021m), yametangazwa majina ya washindi wa shindano la kijana wa Alkafeel lililofanywa katika mwezi wa Ramadhani kwa njia ya mtandao, shindano maalum kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na shule za Iraq, lililo simamiwa na idara ya mahusiano ya vyuo na shule chini ya kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ambalo pia ni sehemu ya mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel.
Kiongozi wa idara ya harakati za vyuo katika idara hiyo Ustadh Muntadhir Swafi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Washiriki wa shindano hili walifika (3876) ambao ni wanafunzi wa vyuo na sekondari (upili), awamu hii imekuwa na muitikio mkubwa kushinda awamu iliyopita, majibu yote yaliwasilishwa kwa kamati ya majaji ambayo iliyachuja na kupata majibu sahihi (611) yaliyo pigiwa kura”.
Akaongeza kuwa: “Upigaji wa kura umefanyiwa ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kupata washindi thelathini”.
Akasema: “Washindi hao thelathini watapewa zawadi maalum pamoja na zawadi nyingine watakayo pewa washiriki wote, sambamba na vyeti vya ushiriki watakavyo pewa baada ya mazingira kuwa vizuri, pamoja na zawadi hizo wenye majibu sahihi watabaki na kuendelea kushiriki kwenye mashindano”.
Akaendelea kusema: Majina ya washindi baada ya kupiga kura yatawekwa pamoja na picha zao, kumbuka kuwa shindano hili ni moja ya mashindano mengi yaliyosimamiwa na idara hii, yanalenga kujenga elimu na utamaduni kwa vijana hao, kupitia maswali yanayo ulizwa kwenye mashindano yanayo lenga pia kunufaika na mwezi huu mtukufu.