Kila siku asiyo asiwa Mwenyezi Mungu ni sikukuu

Maoni katika picha
Sikukuu sio sawa na siku zingine, ni siku tofauti katika kila jambo, ni siku ambayo Mwenyezi Mungu ameiteua kuwa sikukuu kwa waislamu, kwa hiyo siku hiyo inatakiwa watu wafanye mambo yanayo endana na uislamu, uislamu unaangalia sikukuu kwa namna ya pekee, ni siku ya watu kukutana na kumtaja Mwenyezi Mungu na kumuelekea yeye kwa kusoma dua.

Falsafa ya Idul-Fitri tukufu ni siku ya furaha kwa waliowezeshwa na Mwenyezi Mungu kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani, hivyo huwa ni mwanzo wa maisha mapya kwa muislamu, maisha ya kudumu katika ibada na kufanya mambo mema pamoja na kushindana katika mambo ya kheri, kiongozi wa waislamu (a.s) amefafanua jambo hilo pale aliposema: (Hakika ni sikukuu kwa wale ambao Mwenyezi Mungu amekubali funga zao, na swala zao, kila siku ambayo hata asiwa Mwenyezi Mungu ni sikukuu).

Watu wengi hukosea kuifanya sikukuu kuwa siku ya michezo na starehe, sikukuu katika uwelewa wa uislamu ni siku ya ibada na kufanya mambo mema, ni siku ya furaha kwa waliokubaliwa funga zao na siku ya huzuni kwa wale ambao hawakukubaliwa ibada zao, aliye samehewa dhambi zake anafurahi kwa kujikurubisha zaidi kwa Mwenyezi Mungu.

Kutoka kwa Abu Abdillahi (a.s) anasema: (Inapofika asubuhi ya siku ya Idul-Fitri hutokea wito: Nendeni kwenye malipo yenu).

Sikukuu ni kwa yule aliyesamehewa dhambi zake, Imamu Ali (a.s) anasema: (Hakika hii ni sikukuu kwa aliyesamehewa), asiyesamehewa dhambi zake na kukubaliwa ibada zake, anatakiwa awe na huzuni katika siku ya sikukuu! Ahisi fedheha kubwa, anatakiwa atumie muda huo kuomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu kabla ya kuukosa.

Imamu Hassan (a.s) anasema: Sikukuu ni siku ya kufanya ibada sio siku ya kucheza na kustarehe, aliona watu wanacheza na kucheka katika siku ya Idul-Fitri, akasimama na kusema: Hakika Mwenyezi Mungu ameufanya mwezi wa Ramadhani kuwa uwanja wa waja wake, washindane kufanya ibada na kutafuta radhi zake, waliofanya vizuri wamefaulu na waliofanya vibaya wamefeli, ni aibu kubwa kumkuta mtu anacheka katika siku ambayo waliofaulu wanalipwa, na waliofanya vibara wanakosa malipo, kama ikiondolewa pazia mngeona wema wanashughulishwa na mema yao na waovu wanashughulishwa na uovu wao.

Hivyo siku ya sikukuu inapasa kuwa mwanzo mpya wa maisha yetu, imepokewa kutoka kwa kiongozi wa waumini (a.s) katika khutuba yake ya siku ya Fitri, alisema: (Tambueni –enyi waja wa Mwenyezi Mungu- wanaume na wanawake waliofunga huitwa na malaika siku ya mwisho katika mwezi wa Ramadhani: Bishara njema enyi waja wa Mwenyezi Mungu, mmesamehewa dhambi zenu, angalieni mtakua vipi kutokana na mliyofanya).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: