Wawakilishi wa Muthanna wanatoa vifurushi vya chakula kwa familia za mafakiri na wenye kipato kidogo

Maoni katika picha
Wawakilishi wa mawakibu katika mkoa wa Muthanna chini ya kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kupitia maukibu ya Answaru-Imamu Mahadi (a.f), wamegawa idadi kubwa ya vikapu vya chakula kwa familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo.

Kiongozi wa wawakilishi hao bwana Saadi Rahim Abdali ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mawakibu Husseiniyya zilizo chini yetu katika mkoa huu, sawa na mawakibu zilizo kwenye mikoa mingine toka mwanzo wa mwezi wa Ramadhani zimekua zikigawa chakula cha aina tofauti kwa mafakiri na watu wenye kipato kidogo, kwa ajili ya kupunguza ugumu wa maisha yao, kazi hii itaendelea mwaka mzima lakini huongezeka zaidi katika siku kama hizi”.

Kiongozi wa opresheni hii na msimamizi wa maukibu tajwa bwana Haidari Majidi amesema kuwa: “Opresheni hii imefikia familia nyingi, tumeanza kazi ya kugawa chakula baada ya kubaini familia zenye uhitaji na aina ya chakula kinacho takiwa na familia hizo, ni furaha kwetu na kwa wahudumu wetu kutoa msaada huu na kusimama pamoja na familia hizi zilizo kubali kupokea msaada wetu, hakika mawakibu za kutoa huduma ikiwemo maukibu yetu zitaendelea kutoa huduma hii, tunamuomba Mwenyezi Mungu atukubalie”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: