Maahadi ya Quráni tukufu inawapa zawadi wanafunzi wake waliomaliza semina ya sauti za kiarabu

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu/ tawi la Najafu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, inawapa zawadi wanafunzi wake waliohitimu semina ya Quráni iliyo pewa jina la (sifa za sauti za kiarabu), katika hafla iliyofanywa baada ya kumaliza semina.

Hafla ilifunguliwa kwa Quráni tukufu, ukafuata ujumbe wa kiongozi wa tawi la Maahadi hiyo Sayyid Muhandi Almayali, akasisitiza kuwa Maahadi itaendelea kufanya semina za kielimu, hadi sasa idadi kubwa ya wanafunzi wamesha shiriki katika semina za Quráni tukufu, kisha wahitimu wakapewa zawadi pamoja na vyeti vya ushiriki.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya kupitia matawi yake tofauti, inafanya harakati mbalimbali za Quráni tukufu ndani na nnje ya mkoa wa Karbala, kwa lengo la kueneza utamaduni wa kufanyia kazi mafundisho ya Quráni katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: