Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake imetangaza matokeo ya moja ya mashindano yake (Rabiul-Quluub)

Maoni katika picha
Kamati ya majaji wa shindano la (Rabiul-Quluub) lililo simamiwa na Maahadi ya Quráni tawi la wanawake, chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza majina ya washindi katika kikosi cha (waliohifadhi juzuu kumi).

Washiriki wa shindano hilo walikua ni wanafunzi wa Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake, na lilifanywa kwa njia ya mtandao kupitia jukwaa la (Google meet), washindi walikua ni:

Mshindi wa kwanza: Rukiya Haidari Mustwafa.

Mshindi wa pili: Batuli Qutada Muhammad Muhammad Saidi.

Mshindi wa tatu: Amina Muhammad Muhammad Saidi.

Ikumbukwe kuwa shindano lilikua na sehemu tofauti, ambazo ni: (waliohifadhi juzuu tatu, waliohifadhi juzuu tano, waliohifadhi juzuu kumi), kila sehemu inavigawanyo vinavyo lenga kuweka ushindani baina ya wanafunzi, na kushawishi kuendelea kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu, sambamba na kushajihisha zaidi wanafunzi waliofanya vizuri.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tawi la wanawake inalenga kueneza elimu ya Dini katika jamii ya wanawake, ikiwemo elimu ya (Quráni tukufu), na kutengeneza kizazi cha wanawake wenye uwezo wa kufanya tafiti za kielimu katika sekta ya Quráni na fani zake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: