Jumla ya watu (189471) wamefanyiwa ziara kwa niyaba

Maoni katika picha
Idara ya teknolojia na taaluma ya mitandao iliyo chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imesema kuwa dirisha la ziara kwa niyaba lililopo katika mtandao wa kimataifa Alkafeel, limepokea maombi na kufanya ziara kwa niyaba ya watu (189471) ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, watu waliofanyiwa ziara wanatoka ndani na nje ya Iraq.

Kiongozi wa idara hiyo Ustadh Haidari Twalibu Abdul-Amiir amesema: “Mtandao wa kimataifa Alkafeel katika kila msimu wa ibada ikiwa ni pamoja na mwezi wa Ramadhani huandaa ratiba ya kiibada kupitia dirisha la ziara kwa niyaba, katika mwezi huu mtukufu tulikuwa na ratiba yenye zipengele tofauti, aidha kulikuwa na ongezeko kubwa la watu waliojisajili katika ukurasa wa ziara kwa niyaba, huduma ya kufanya ziara kwa niyaba ilianza tangu siku ya kwanza katika mwezi wa Ramadhani hadi siku ya Idilfitri tukufu”.

Akafafanua kuwa: “Watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu ambao ni masayyid wamefanya asilimia kubwa ya ibada hizo kwa kushirikiana na idara ya Swafha, ukitoa ziara ya Imamu Hassan (a.s) katika mji wa Madina na ziara ya kiongozi wa waumini (a.s) katika mji wa Najafu zilizo fanywa na watu wakujitolea”.

Akaongeza kuwa: “Ratiba ya ibada ilihusisha:

  • - Ziara ya kila siku ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
  • - Usomaji wa Quráni uliosimamiwa na Maahadi ya Quráni tukufu katika Atabatu Abbasiyya.
  • - Baadhi ya ibada maalum za mwezi huu, ikiwa ni pamoja na kusoma dua ya Iftitaah na zinginezo zinazo suniwa kusomwa katika mwezi wa Ramadhani.
  • - Ziara maalum ya Imamu Hassan Almujtaba (a.s) katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwake huko Madina jirani na kaburi lake takatifu.
  • - Ibada maalum za siku za Lailatul-Qadri.
  • - Ziara maalum ya kiongozi wa waumini (a.s) katika kumbukumbu ya kifo chake”.

Hitimisho la ratiba hiyo ilikua ni kufanya ziara maalum ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika usiku wa Iddi na mchana wake.

Kumbuka kuwa kufanya ziara kwa niyaba ni moja ya huduma muhimu inayo tolewa na mtandao wa kimataifa Alkafeel, jumla ya maombi milioni moja na laki moja na elfu sitini na nane mia sita na nane (1,168,608) yamepokelewa mwaka jana kutoka nchi tofauti duniani, kupitia mitandao yake ya (kiarabu – kiengereza – kifarisi – kituruki - kiurdu – kifaransa – kiswalihi – kijerumani).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: