Kuongeza kipindi cha kupokea kazi zinazo shiriki kwenye shindano la kusoma surat Faatihah

Maoni katika picha
Kamati inayosimamia (shindano la Baraaim) la usomaji wa surat Faatihah kwa usahihi imetangaza kuongeza muda wa kupokea kazi zitakazo shiriki kwenye shindano hilo (Ahmadi na mwezi) hadi Jumatano (6 Shawwal 1442h) sawa na (19 Mei 2021m).

Kiongozi wa uhusiano wa vyuo na shule chini ya kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Maahir Khalidi amesema: “Tumeongeza muda kwa ajili ya kutoa wakati mrefu kwa washiriki, sambamba na kupokea simu kutoka kwa washiriki walio omba kuongezewa muda ili waweze kukamilisha kazi zao”.

Akaongeza kuwa: “Shindano halijaweka badiliko lolote katika masharti yake, ambayo ni:

  • - Mshiriki atume kazi yake pamoja na wasifu (cv) yenye majina yake matatu na namba ya simu yake.
  • - Mshiriki awe na umri chini ya miaka (15).
  • - Sauti isikike vizuri.
  • - Asome taratibu sio haraka haraka.
  • - Muda usizidi dakika moja.
  • - Rekodi yake ya sauti aitume kwaye namba ya simu ifuatayo (07602306524 kwa telegram).

Kumbuka kuwa hili ni moja ya mashindano muhimu ya kielimu, aidha ni moja ya kazi muhimu ya kutengeneza katuni za kufundishia, itakayo saidia kutambua sehemu ambazo hukosewa na watu wengi pamoja na usahihi yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: