Haafidhwah kutoka Ataba tukufu amekua mshindi wa kwanza katika shindano la (Anwaarul-Khaatam)

Maoni katika picha
Mmoja wa wanafunzi wa Maahadi ya Quráni tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, amekuwa mshindi wa kwanza kwenye shindano la (Anwaarul-Khaatam) la Quráni lililofanywa katika mwezi wa Ramadhani, chini ya ofisi ya ufundishaji wa Quráni katika idara ya tablighi upande wa wanawake katika Atabatu Husseiniyya tukufu.

Mwanafunzi Dhuha Hussein Halo amewashinda wenzake walio hifadhi juzuu ishirini kutoka ndani na nje ya Iraq katika shindano hilo.

Kiongozi wa Maahadi bibi Manara Jaburi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hii sio mara ya kwanza wanafunzi wetu wa Maahadi kupata ushindi, wamesha pata ushindi kwenye mashindano tofauti waliyo shiriki siku za nyuma, jambo hili linaonyesha ubora wa mfumo wa ufundishaji unaotumiwa na Maahadi na idara zake, pamoja na msaada unaotolewa na Atabatu Abbasiyya kwenye sekta hii”.

Akaongeza kuwa: “Pamoja na kwamba shindano limefanywa kwa njia ya mtandao lakini lilikua na ushindani mkali, kwa bahati nzuri mwanafunzi wetu ameshinda, ushindi huu ni matokeo ya kazi kubwa inayo fanywa na wakufunzi wetu pamoja na juhudi ya mwanafunzi mwenyewe, pamoja na kujengeka moyo ya ushindani katika kuhifadhi Quráni tukufu”.

Kumbuka kwa wanafunzi wa Maahadi hii wamesha shiriki kwenye mashindano mengi, na wamesha pata nafasi za juu kwenye mashindano hayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: