Kwa kuhudhuria na njia ya mtandao: kitengo cha Dini kimefanikiwa katika ratiba yake ya mwezi wa Ramadhani

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza kufanikiwa ratiba ya mwezi wa Ramadhani mtukufu iliyotekelezwa kwa mahudhurio ya moja kwa moja na kwa njia ya mtandao, katika sekta ya tablighi na utamaduni, ratiba ya mwaka huu ilizingatia uwepo wa janga la virusi vya Korona na changamoto zake.

Makamo rais wa kitengo hicho, Shekh Aadil Wakiil amesema kuwa: “Pamoja na changamoto zilizopo kitengo chetu kiliweka ratiba na kikaitekeleza, kwa ajili ya kunufaika na siku za mwezi huu mtukufu kwa kuelekeza na kuongeza maarifa ya watu wanaokuja kufanya ziara”.

Akaongeza kuwa: “Kitengo kimefanya mambo tofauti yanayo husiana na maelekezo ya Dini pamoja na utamaduni, yanayo endana na utukufu wa mwezi huu, kimeendesha mambo yake kupitia mitandao ya mawasiliano ukiwemo mtandao wa kimataifa Alkafeel, na matangazo ya moja kwa moja (mubashara) kupitia vyombo mbalimbali vya habari, kwa kutumia masafa iliyo tengenezwa na kituo cha uzalishaji wa vipindi Alkafeel chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, asilimia kubwa ya shughuli zetu tumezifanya kwa kushirikiana na kitengo cha habari, kitengo hicho kilikuwa na mchango mkubwa wa kufanikisha shughuli zetu”.

Akaendelea kusema: “Tuliweka vituo vya kujibu maswali yanayo husu Fiqhi, Aqida na Akhlaq, na kutoa maelekezo kwa watu wanaokuja kumzuru Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na kufungua milango ya mawasiliano ya simu”.

Tambua kuwa lengo la kuandaa ratiba hii ni kwa ajili ya kunufaika na mwezi huu mtukufu, kwa kufanya mambo sahihi, chini ya bendera ya Dini takatifu tuliyo husiwa na Mtume (s.a.w.w) tushikamane nayo, na kunufaika na kipindi kizuri kwa kufanya ibada na kuomba dua.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: