Kiwanda cha kutengeneza barafu Alkafeel kimetengeneza na kugawa mamia ya vipande vya barafu ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani

Maoni katika picha
Idara ya kiwanda cha kutengeneza barafu Alkafeel kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kuwa imefanikiwa kutengeneza mamia ya vipande vya barafu na kuzigawa bure ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, kiwango cha uzalishaji wa barafu kiliongezeka kutokana na kuongezeka kwa joto na mahitaji ya barafu.

Kiongozi wa kiwanda Mhandisi Farasi Mirza Salmani ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tumekua tukitengeneza barafu na kugawa kwa zaidi ya miezi miwili, kutokana na kuingia mwezi mtukufu wa Ramadhani katika msimu wenye joto kali kulisababisha kuongezeka kwa mahitaji ya bidhaa hiyo kwenye mawakibu na kwa mazuwaru, tukaanza kuwafikishia barafu kwa kutumia gari za kiwanda, uzalishaji na usambazaji ulikua unaongezeka kila siku hususan katika kumi la pili la mwezi mtukufu wa Ramadhani”.

Akabainisha kuwa: “Barafu na maji yalisambazwa katika maeneo tofauti, miongoni mwa maeneo hayo ni:

  • - Kituo cha kugawa maji kinacho sambaza maji baridi ya kunywa katika Atabatu Abbasiyya tukufu na kwa mazuwaru wake.
  • - Mawakibu Husseiniyya zianazo hudumia mazuwaru.
  • - Majengo yanayo tumika kutoa huduma yaliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
  • - Vitengo vya Atabatu Abbasiyya na maeneo yaliyo jirani yake.
  • - Kwenye vituo vya askari ndani ya Mji mtukufu wa Karbala”.

Kumbuka kuwa kiwanda kipo chini ya shirika la kiuchumi Alkafeel, huwa na mchango mkubwa wakati wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, aidha hufanya kazi nyingi za nje, ikiwa ni pamoja na kugawa maji na barafu kwenye ziara zinazo fanywa katika Ataba zingine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: