Mwezi tano Shawwal balozi wa Imamu Hussein awasili katika mji wa Kufa

Maoni katika picha
Mji wa Kufa katika siku kama ya leo mwezi tano Shawwal mwaka wa 60 hijiriyya, balozi wa Imamu Hussein (a.s) na mtoto wa Ammi yake Muslim bun Aqiil (a.s) aliwasiri katika mji huo kuangalia hali ya wakazi wa mji huo na msimamo wao ili amjulishe ndugu yake kwa ajili ya kufanya maamuzi.

Alifanya hivyo baada ya kumiminika barua za watu wa Kufa kwa Imamu Hussein (a.s) zinazo muomba aende katika mji huo kuwaokoa katika dhulma za bani Umayya, baadhi ya barua hizo zilikua zinambebesha wajibu mbele ya Mwenyezi Mungu katika umma.

Ndipo Imamu akaona kabla ya kufanya maamuzi yeyote amtume balozi wake kwao, atakaye mjulisha ukweli wao na uaminifu wao kwake (a.s), akiwaona wanania ya kweli achukue kiapo cha utii kwao, baada ya hapo ndio yeye afunge safari ya kwenda katika mji huo, Imamu (a.s) alichagua mtu muaminifu zaidi kwake na mkubwa kwa umri katika watu wa nyumba ya Mtume (a.s) Muslim bun Aqiil, naye alikubali na kuridhia kwa moyo mmoja jukumu hilo, akampa barua isemayo: (Kutoka kwa Hussein bun Ali kwenda kwa kila atakaefikiwa na barua hii katika viongozi na wafuasi wangu katika wa mji wa Kufa: Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yenu, Amma baad: Zimenijia barua zenu, zinazo onyesha mapenzi yenu ya ujio wangu kwenu, na mimi namtuma kwenu ndugu yangu mtoto wa Ammi yangi, mtu ninae muamizi zaidi katika familia yangu Muslim bun Aqiil, ili anijulishe jambo lenu na aniandikie atakayo yaona kwenu, kama mkiwa sawa na zinavyosema barua zenu na wajumbe wenu walio nijia, nitakuja haraka kwenu kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu).

Muslim akachukua barua na akaondoka Maka usiku wa mwezi kumi na tano Ramadhani, akapita Madina na kuswali katika msikiti wa Mtume (s.a.w.w) kisha akazunguka kaburi la Mtume na akawaaga watu wa familia yake, halafu akaanza safari ya kwenda Iraq.

Akafikia katika nyumba ya Mukhtaaru bun Ubaida Athaqafi, watu wakaanza kumiminika kwake, kila wakikusanyika anawasomea barua ya Imamu Hussein (a.s) huku wanalia kwa mapenzi na furaha, kisha wanatoa kiapo cha utii, hadi idadi ya watu waliotoa kiapo cha utii ikafika elfu kumi na nane, baada ya kufika idadi hiyo kubwa akaona mazingira hayaruhusu kuchelewa Imamu kuja katika mji huo, ndipo Muslim akamuandikia barua Imamu Hussein (a.s), isemayo: (Amma Baad.. Hakika mjumbe hadanganyi watu wake, watu wote wa Kufa wako pamoja na wewe, wametoa kiapo cha utii watu elfu kumi na nane, baada ya kukufikia barua hii njoo haraka wasalam).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: