App ya Alkafeel ni njia rahisi ya kuwasiliana na Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
App ya (mtandao wa kimataifa Alkafeel) inayofanya kazi katika simu za kisasa zenye (Android & los) ni moja ya njia rahisi ya kuwasiliana na Atabatu Abbasiyya tukufu, na kuangalia harakati zake, aidha ni sehemu ya mawasiliano ya kudumu kiroho, kifikra na kitamaduni.

App hiyo imeandaliwa na kusanifiwa na wataalam wanaofanya kazi katika kitengo cha habari cha Atabatu Abbasiyya tukufu, inauwezo mkubwa na rahisi kuitumia kwa kuangalia vitu vilivyomo kwa urahisi kabisa.

Kiongozi wa idara hiyo Ustadh Haidari Twalibu Abdul-Amiir amesema: App hii imetengenezwa mwaka (2012) inatoa huduma kila sehemu ya dunia, ni rahisi kuitumia katika kuangalia harakati za Ataba tukufu katika sekta ya (utamaduni, elimu, ujenzi na zinginezo…) chini ya teknolojia ya kisasa kabisa duniani.

Akaongeza kuwa: “App inapatikana katika simu za kisasa, nayo ni sawa na toghuti ya kimataifa Alkafeel, kwani inamilango mingi, miongoni mwa milango yake ni: (habari – matangazo mubashara – maktaba ya picha – maktaba ya video – khutuba za Ijumaa..) aidha inajenga mawasiliano ya kiroho kupitia ukurasa wa ziara kwa niyaba, ambao watu hujiandikisha na kufanyiwa ziara kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na ziara katika Ataba zingine za ndani na nje ya Iraq, hali kadhalika kuna mlango wa barua kwa Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akasisitiza kuwa: “Tangu kuanzishwa kwa App hii imekua ikifanyiwa maboresho mbalimbali, bado inaendelea kufanyiwa maboresho ili kuifanya kuwa ya kisasa zaidi katika uwanja wa App, inasaidia kufikisha sauti ya Atabatu Abbasiyya mbali na huduma inazo toa”.

Kumbuka kuwa App inapatikana kwenye:

  • - (Google Play) katika simu zenye (Android).
  • - (Apple Store) katika simu zenye (ios).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: