Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Hindiyya chini ya Atabatu Abbasiyya imehitimisha shindano la kwanza la usomaji wa Quráni, ambalo wasomaji kadhaa wa tawi hilo wameshiriki.
Shindano limefanywa kwatika mji wa Hindiyya, katika mzunguko wa mwisho wameshiriki wasomaji kumi na moja, ushindani mkubwa umeshuhudiwa kati yao, na hatua ya mwisho yametangazwa majina ya washindi watatu wa mwanzo.
Tambua kuwa kanuni za kujikinga na maambukizi zimezingatiwa kwenye shindano hili ikiwa ni pamoja na umbali kati ya mtu na mtu katika ukaaji, aidha shindano hili limesaidia kujenga moyo wa ushindani baina yao, kwa ajili ya kujiandaa kushiriki mashindano mengine ya kieneo na kitaifa.
Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu ni moja ya vituo muhimu katika kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, inalenga kusambaza elimu ya Quráni na kutengeneza jamii yenye uwelewa na maarifa ya Quráni katika sekta zote.