Kuisha kwa shindano la (Taaju-Khudaam)

Maoni katika picha
Idara ya tablighi chini ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, siku ya Jumatano imefanya hafla ya kuhitimisha shindano lililofanywa katika mwezi wa Ramadhani upande wa wanawake lililo husisha watumishi wa Ataba tukufu, na kupewa jina la (Taaju-Khudaam), lililofanyiwa ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s).

Hafla imefunguliwa kwa Quráni tukufu iliyo somwa na Liith Ubaidi, ukafuata ujumbe kutoka idara ya tablighi ulio wasilishwa na kiongozi wa idara hiyo Sayyid Muhammad Mussawi, amesema: “Shindano hili limefanywa kwa mwaka wa kumi mfululizo, limepata ushiriki mkubwa wa watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), jumla ya watu elfu nane wameshiriki kwenye shindano hili, asilimia kubwa wamefanya vizuri”.

Akaongeza: “Shingano hili ni njia ya kupata maarifa, linalenga kujenga uwezo wa watumishi kielimu, akasisitiza umuhimu wa kufanya harakati mbalimbali ndani na nje ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kama vile kufanya mashindano, kutoa mihadhara, kuandika na mengineyo, miongoni mwa harakati hizo ni shindano hili”.

Baada ya hapo ukafuata ujumbe kutoka kwa watumishi walioshiriki, ulio wasilishwa kwa niyaba yao na Hussein Fahim, ameushukuru uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya na Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, akaomba ziendelee kufanywa semina zaidi na mashindano yanayo lenga kujenga uwezo wa watumishi.

Mwisho kabisha zawadi zikatolewa kwa washindi sambamba na kutoa shukrani rasmi kwa rais wa kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu Shekh Swalahu Karbalai, pamoja na kubainisha nafasi ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na Ahlubait wengine (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: