Msimamizi wa shindano hilo Ustadh Amru Alaa ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Shindano hili ni kwa ajili ya kuonyesha filamu hii na kunufaika kutokana na mafundisho yake, aidha limesaidia kuongeza moyo wa ushindani baina ya washiriki na wengineo”.
Akaongeza kuwa: “Pamoja na muda waliopewa washiriki kuwa mfupi, na ugeni wa shindano hili kwa sababu halijawahi kufanywa hapo kabla, lakini limepata mwitikio mkubwa, baada ya kupokea kazi za washiriki kamati ya majaji imezigagua na kuzichuja zilizo kamilisha masharti ya shindano, kisha zilizo gongana zikapigiwa kura mbele ya rais wa kitengo na kiongozi wa idara ya miradi ya Quráni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na kupata washindi kumi wafuatao:
- 1- Zaidu Hashim Naaji.
- 2- Zuhura Mahmuud Shaakir.
- 3- Muhammad Usama Abdulhamza.
- 4- Sajaad Hussein Shaakir.
- 5- Muhammad Fadhili Ibrahim.
- 6- Zaharaa Ali Kaadhim.
- 7- Abuu Hassan Yasini Kariim.
- 8- Narjisi Bashiri Muhammad.
- 9- Batuli Abduljabbaar Numi.
- 10- Fatuma Ali Abduraufu”.
Akabainisha kuwa: “Washindi watano wa kwanza wamepewa zawadi za kifaa cha (tablet) kwa kila mmoja, na watono walibaki kila mmoja amepewa msahafu unao ongea (Quránu-Naadwiq)”.
Kumbuka kuwa filamu ya (Ahmadu na mwezi) ni filamu ya kwanza ya kufundisha kisomo sahihi cha surat Fat-hah, imeandaliwa na watumishi wa kituo cha Aljuud chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya.