Kazi ya usafi inafanywa kila siku katika maeneo yanayo zunguka Ataba tukufu

Maoni katika picha
Idara ya usafi chini ya kitengo cha utumishi, inaendelea kutekeleza jukumu lake la kusafisha barabara zinazo zunguka Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kiongozi wa idara ya usafi bwana Muhammad Ahmadi Jawadi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika watumishi wa idara hii hawapumziki kudeki na kusafisha maeneo yanayo zunguka Atabatu Abbasiyya au barabara zinazo elekea kwenye Ataba hiyo”.

Akaongeza kuwa: “Vitendea kazi vya idara vinatumika muda wote, huwekwa utaratibu wa kufagia na kudeki kulingana na harakati za mazuwaru”.

Akaendelea kusema: “Kazi zetu zinaendelea kila siku hadi katika maeneo ya chini ya ardhi, watumishi wetu huandaa kumbi zilizopo katika tabaka la jinni kwa ajili ya kutumiwa na mazuwaru, husafishwa na kupulizwa dawa mfululizo”.

Akasema: “Watumishi wetu pia huandaa sehemu za kuswali mazuwaru katika maeneo yanayo zunguka Ataba tukufu, sambamba na kuandaa sehemu za kufanyia majlisi za kuomboleza na kutolea mihadhara ya kidini”.

Kumbuka kuwa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ni miongoni mwa vitengo vinavyo toa huduma ya moja kwa moja kwa mazuwaru, na kinafanya kila kiwezalo kuhakikisha kinatoa huduma bora zaidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: