Maahadi ya Quráni tukufu katika mji wa Najafu imetangaza semina mpya

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Najafu chini ya Atabatu Abbasiyya, imetangaza ufunguzi wa semina ya Quráni katika hukumu za tajwidi.

Ratiba ya semina ipo kama ifuatavyo:

  • - Semina itaanza siku ya Jumapili (23/05/2021).
  • - Mihadhara itatolewa siku ya Jumapili na Jumatano kila wiki, saa mbili jioni.

Masharti ya kujiunga na semina ni:

  • 1- Mshiriki awe na umri wa miaka (17) na kuendelea.
  • 2- Usajili unafanywa kwa kujaza fomu ya kielektronik kwenye mtandao kupitia link ifuatayo: https://forms.gle/aA3FDJWbpXVS9tu27

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu kupitia matawi yake tofauti ni sehemu muhimu ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, inalenga kusambaza elimu ya Quráni na kutengeneza jamii yenye kufanyia kazi mafundisho ya Quráni na uwezo wa kufanya tafiti za kielimu katika sekta tofauti kuhusu Quráni tukufu na fani zake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: