Miaka kumi tangu kufunguliwa toghuti ya kwanza maalum kuhusu tukio la Baqii

Maoni katika picha
Idara ya teknolojia na taaluma chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu miaka kumi iliyopita, yaani mwaka wa 1432h. ilitengeneza toghuti ya kwanza kwa jina la (Baqii Gharqad). Ikiwa ni toghuti maalum kwa ajili ya kuangazia tukio la kuvunjwa makaburi ya Baqii na mazaru ya Maimamu (a.s) wa Baqii, ikiwa ni katika kumbukumbu ya mwaka wa themanini na nane tangu kuvunjwa kwa makaburi hayo na mazaru za Maimamu (a.s).

Toghuti hiyo ilizinduliwa kwa hafla kubwa iliyofanywa ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) iliyohudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria –katibu mkuu wa kipindi hicho- Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na wawakilishi wa ofisi za Maraajii Dini kutoka Najafu, bila kuwasahau wawakilishi wa Ataba na viongozi wa Dini pamoja na wawakilishi wa makundi ya utamaduni, sekula na habari.

Toghuti hiyo ni mchango wa Atabatu Abbasiyya katika kuangazia tukio la kubomolewa makaburi ya Maimamu wa Baqii na yaliyotokea wakati huo na yanayo endelea kutokea hadi sasa, na kutoa nafasi kwa kila mtu aweze kuangalia sehemu hiyo takatifu popote alipo duniani, toghuti hiyo imekuwa ikiboreshwa na kutafsiriwa kwa lugha ya kiengereza, inamilango mingi. Kunamilango ya kitamaduni, kitumishi ambayo inaangazia maisha ya Maimamu wanne (a.s) ambao ni: (Mujtaba – Sajjaad – Baaqir – Swaadiq), na tukio la kubomolewa makaburi ya Baqii pamoja na historia ya jina la Baqii Gharqad na maswahaba waliozikwa hapo pamoja na ziara kwaniyaba na ukurasa wa picha za mnato na video.

Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi aliongea katika hafla hiyo akabainisha kuwa: “Vyombo vya habari vinalazimika vibebe jukumu la kusema ukweli nalo ni jukumu kubwa, kuna watu hawajui ukweli ni lazime waupate kutoka kwenye vyombo vya habari wanavyo viamini, kunawengine bado wanawasiwasi na habari walizonazo wanahitaji kuthibitisha kupitia vyombo vya habari, kwa hakika hilo ni jukumu la vyombo vya habari viaminifu, haki hauwezi kuificha, inaweza kuchelewa baadhi ya wakati lakini lazima itadhihiri, ndipo likaja wazo la kuanzisha toghuti ya Baqii kwa ajili ya kuangazia mambo yaliyo tokea katika eneo hilo”.

Akabainisha kuwa: “Toghuti haiwezi kufanikiwa ispokua kwa juhudi za waandishi wa habari watakao kusanya taarifa, tunatoa wito kwa kila mwenye taarifa zinazo husu Baqii azitoe, toghuti itaziandika na kuzitangaza”.

Kuangalia toghuti fungua link ifuatayo: https://alkafeel.net/albaqee/
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: