Kuratibu zaidi ya vikao mia moja vya usomaji wa Quráni ndani ya mwezi mmoja

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeratibu zaidi ya vikao (100) vya usomaji wa Quráni ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, usomaji huo umefanywa ndani ya ofisi za makao makuu ya Maahadi katika mji wa Najafu na kwenye matawi na vituo mbalimbali vilivyopo mikoani, sambamba na kutekeleza masharti yote ya kujikinga na maambukizi.

Mkuu wa Maahadi Sayyid Mannaar Jaburi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Usomaji huo umefanywa wakati wa mazingira magumu kutokana na kuwepo kwa maambukizi ya virusi vya Korona, lakini tumefanikiwa kuratibu idadi hiyo kubwa ya visomo vya Quráni, na kunufaika na mwezi huo mtukufu ambao huzingatiwa kuwa ni msimu wa Quráni, Usomaji huo umefanywa ndani ya Husseiniyya mbalimbali na kwenye nyumba za watu, chini ya usimamizi wa wasomaji mahiri wa Quráni”.

Akabainisha kuwa: “Vikao vya usomaji wa Quráni, havikuishia kwenye usomaji wa Quráni peke yake, bali kulikuwa na vipengele vingine, kama vile kubainisha maana za baadhi za aya na hukumu zake, mashindano ya Quráni na mihadhara, tunamshukuru Mwenyezi Mungu muitikio wa washiriki ulikuwa mkubwa pamoja na kulazimika kuwa na washiriki wachache kwa ajili ya kuhakikisha wanakaa kwa umbali unaokubalika kiafya”.

Kumbuka kuwa vikao vya usomaji wa Quráni vimedumu mwezi mzima, na vililenga kunufaika na mwezi huo mtukufu, na kuhimiza jamii ipende kusoma Quráni na fani zake sambamba na kusambaza utamaduni wa kusoma Quráni katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: