Kukamilika kwa utengenezaji wa vipande vya dirisha la Maqaam ya mkono na maandalizi ya kuvifunga yanaendelea

Maoni katika picha
Kitengo cha kutengeneza madirisha ya kwenye makaburi matakatifu na milango chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimesema kuwa, mafundi wake wamemaliza kazi ya kutengeneza vipande vya dirisha la Maqaam ya mkono wa kushoto wa Abulfadhil Abbasi (a.s), hivi sasa yanafanyika maandalizi ya kuviweka kwenye Maqaam hiyo iliyopo nje ya Ataba tukufu, jirani na mlango wa kiongozi wa waumini (a.s).

Kazi hii inaingizwa katika orodha ya mafanikio yaliyopatikana ndani na nje ya Iraq, mafanikio haya yamefanywa na raia wa Iraq.

Rais wa kitengo cha kutengeneza madirisha na msimamizi mkuu wa kazi hiyo Sayyid Naadhim Ghurabi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Watumishi wa kitengo wamekamilisha utengenezaji wa vipande vya kuweka kwenye dirisha hilo ndani ya muda uliopangwa na kwa ubora mkubwa, pamoja na kuwa na kazi nyingi kwenye miradi mingine, kama vile mradi wa dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s), kutengeneza sura ya mbele ya malalo ya Imamu Mahadi (a.f) upande wa wanawake, kazi hizo hazikuzuwia utendaji katika dirisha hili tukufu, tayali vipande vyote vya madini na vya mbao vimekamilika, vinatarajiwa kufungwa kwenye dirisha hivi karibuni kama ilivyo pangwa”.

Akaongeza kuwa: “Kazi ya mwisho iliyofanywa katika mradi wa dirisha hili ni kuchovya dhahabu na mina ya kijani vipande vyenye maandishi ya Quráni na mashairi, pamoja na vipande vya mapambo (Alkalwa), vipande vyenye maandishi ya Quráni na mapambo vipo kama ifuatavyo:

Kwanza: vipande vya maandishi ya Quráni kinaurefu wa (sm 20) vipo vipande nane na vinazunguka dirisha sehemu zote, vimeandikwa aya zilizopo katika surat Mutwafifiin (Innal-Abraara lafii naiim…) hadi (Alal-Araaiki yandhuruuna) herufi za dhahabu iliyotiwa mina ya bluu, kwa juu ya herufi hizo kuna ufito wa pambo wenye urefu wa (sm 6).

Pili: ufito wa (maandishi ya shairi) wenye urefu wa (sm 20), miongoni mwa tungo za Saffaar, umezunguka dirisha lote, herufi zake zinadhahabu iliyotiwa mina ya kijani.

Tatu: ufito wa pambo unao zunguka sehemu zote nane za dirisha, unaurefu wa (sm 28), kila kipande kinapambo la uwa lenye umbo la duara, jumla yapo (16), kila sehemu inatenganishwa na nyingine kwa ufito wa fedha, uliopo kwenye nguzo zote nane na katika eneo linalo tenganisha maandishi ya Quráni na shairi”.

Kumbuka kuwa dirisha linaumbo la pembe nane, nalo ni dirisha la kwanza kutengenezwa kwa umbo hili, ukubwa wa mzunguko wake ni (mt 3) na urefu wake ni (mt 2.85), umbo lake limetengenezwa kwa sifva yenye ujazo wa (ml 2), limebuniwa na kutengenezwa kwa umaridadi na uimara mkubwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: