Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake inapongeza washindi wa mashindano ya Quráni

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya hafla ya kuwapongeza washindi wa mashindano ya Quráni yaliyofanywa ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Hafla imefanywa ndani ya kumbi za makao makuu ya Maahadi katika mkoa wa Najafu, wameshiriki watumishi wa Maahadi na wasimamizi wa mashindano hayo pamoja na walioshiriki kwenye mashindano.

Kiongozi wa Maahadi bibi Mannaar Jaburi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Leo tumefanya hafla ya kuwapongeza watu waliopata ushindi kwenye mashindano tuliyofanya ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, mashindano yaliyo husisha makundi tofauti ya wanawake na kupata mwitikio mkubwa”.

Akaongeza kuwa: “Hafla hii ni fursa ya kuwakutanisha wasomi wa Quráni na kuwapongeza, tunatarajia kufanya hivi zaidi kwa ajili ya kujenga moyo wa ushindani na kuonyesha vipaji na uwezo wa wasomi wetu wanaofaa kuwa kiigizo chema kwa mabinti zetu na katika jamii ya wanawake kwa ujumla, tunawapongeza kwa mafanikio haya pamoja na kuipongeza idara na walimu waliosimamia mashindano hayo ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, kwa lengo la kueneza utamaduni wa usomaji wa Quráni”.

Akafafanua kuwa: “Tulisimamia jumla ya mashindano sita, ambayo ni:

Kwanza: shindano la kisa cha aya.

Pili: shindano la Lu-u lu-u Manshuur.

Tatu: shindano la Duru-Maknuun.

Nne: mashindano ya Quráni katika kila wiki ndani ya mwezi wa Ramadhani.

Tano: matokeo ya shindano la (Rabiul-Quluub).

Sita: shindano la kuhifadhi surat Israa.

Mashindano hayo ni sehemu ya harakati za mwezi mtukufu wa Ramadhani, tunatarajia kuongeza idadi yake siku za mbele”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: