Shindano la Quráni ambalo wameshiriki washindani (230) kutoka ndani na nje ya Iraq limeisha

Maoni katika picha
Kitengo cha masomo ya Quráni katika chuo kikuu cha Ummul-Banina (a.s) kimekamilisha shindano lililo endeshwa kwa njia ya mtandao na kuhusisha wanawake chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, shindano la Quráni la pili liitwalo (Mimi nipo karibu) maalum kwa dua za Quráni, likiwa na washindani (230) kutoka ndani na nje ya Iraq.

Rais wa kitengo katika chuo Ustadh Ali Bayati ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hili shindano la Quráni katika mtindo huu ni la pili, nalo ninalenga kubaini dua zilizopo ndani ya Quráni tukufu, mashindano ya aina hii ni machache sana ndani na nche ya Iraq, mashindano haya yanaumuhimu mkubwa katika jamii, hasa kwa wale ambao hawawezi kuhifadhi Quráni nzima kutokana na shughuli au uwezo wa kufanya hivyo”.

Akaongeza kuwa: “Shindano limeendeshwa kwa njia ya mtandao na kupata washiriki (230) kutoka mikoa (12) ya Iraq, pamoja na wengine kutoka nchi zingine kama vile Sirya, Lebanon, Kuwait, Saudia na Swiden”.

Akabainisha kuwa: “Baada ya mchujo tukapata washiriki (77) waliopata (%100) baada ya kusikilizwa na kamati ya majaji, kamati ilikua imeandaa zawadi za washindi (3) wa mwanzo, ikabidi ipigwe kura ili kupata washindi hao, baada ya kura wakafanikiwa kushinda wafuatao: Raghad Haamid/ kutoka Bagdad, Rugayya Abdulhussein/ kutoka Bagdad, Nadhmiyya Abdullah/ kutoka Karkuuk”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: