Warsha ya mafunzo ya kujikinga na kemikali

Maoni katika picha
Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kamati ya elimu/ idara ya maabara, kinatoa mafunzo ya namna ya kujikinga na madhara ya kemikali kwa watumishi wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mmoja wa wahadhiri wa warsha Ustadh Wasim Twalib Mahadi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Warsha hii inafanywa kwa ajili ya kuwajulisha watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wanaofanya kazi zinazo husiana moja kwa moja na kemikali, namna ya kujilinda na kemekali hizo, ambazo huwa na madhara makubwa kwa afya ya mwanadamu kama zikitumiwa vibaya”.

Akaongeza kuwa: “Mafunzo yanalenga kulinda afya za watumishi na kutambulisha aina tofauti za kemikali wanazo tumia mara kwa mara, sambamba na kuongeza uwezo wa watumishi hao katika kuamiliana na kemikali pamoja na kujiepusha na madhara yake”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu hufanya warsha na semina mbalimbali kwa ajili ya kujenga uwezo wa watumishi wake kwenye sekta tofauti katika vitengo, vituo na taasisi zake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: