Chuo kikuu Al-Ameed: tumefanikiwa kutumia mitandao ya kielektronik ya kimataifa kuwafikishia wanafunzi wa chuo mada za masomo

Maoni katika picha
Rais wa chuo kikuu cha Al-Ameed Dokta Muayyad Imran Ghazali amesema: “Tumepata mafanikio makubwa ya kuwatumia wanafunzi wetu mada za masomo kupitia mitandao ya kimataifa, ambayo mwanafunzi amesoma kama vile yupo kwenye ukumbi wa darasa”.

Akaendelea kusema kwenye ujumbe aliotoa katika kongamano la kimataifa kuhusu ufundishaji kwa njia ya mtandao: “Chuo kikuu Al-Ameed kimejikita katika ufundishaji wa kutumia mitandao baada ya kukamilisha vitendea kazi vya lazima na kuandaa wataalamu, kitengo hicho ni muhimu sana katika chuo kama ilivyo kwenye vyuo vikuu vya nchi zilizo endelea duniani”.

Akafafanua kuwa: “Baada ya kutokea janga la virusi vya Korona na kusimama uhudhuriaji wa wanafundi madarasani tulilazimika kutumia mitandao katika ufundishaji, tukaandaa kompyuta na wataalamu kwa ajili ya kuhakikisha wanafunzi wanafundishwa kama ilivyo pangwa kwenye selebasi ya masomo ya mwaka (2019 – 2020)”.

Akasisitiza kuwa: “Tunamshukuru Mwenyezi Mungu, taarifa ya kamati ya wizara iliyo tembelea chuo chetu inaonyesha tumefanikiwa, walikagua utaratibu tunaotumia katika ufundishaji, wakaupongeza na kuusifu kwa kufikia malengo yanayo kusudiwa na kwamba njia hiyo imedumisha mawasiliano kati ya wakufunzi na wanafunzi”.

Akamaliza kwa kusema: “Somo hufafanuliwa kwa kutumia mitandao tofauti ya mawasiliano kupitia majukwaa ya kisasa katika ufundishaji, pamoja na madarasa ya kwenye mitandao ya kisasa, yaliyo andaliwa na chuo kuwezesha utaratibu huo, yamesaidia kwa kiwango kikubwa utowaji wa elimu bora”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: