Toleo la kumi na nane la jarida la (Radu-Shamsi)

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Hilla chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimechapisha toleo la kumi na nane la jarida la (Radu-Shamsi), linalo andika kuhusu turathi za Hilla, toleo hilo linamakala za turathi na historia ya mji wa Hilla, limeandika vitu vingi katika kurasa (110).

Rais wa wahariri wa jarida hilo Shekh Swadiq Khawilidi amesema kuwa: “Jarida la (Radu-Shamsi) limebeba jina la sehemu ambayo kiongozi wa waumini (a.s) alifanya muujiza wa kurudisha jua, linaandika aina tofauti za turathi za Hilla, kuanzia historia ya wanachuoni watukufu wa mji huo na makaburi yao, pamoja na vitu vya kihistoria vilivyopo katika mji, linaonyesha hali ya zamani na ya sasa katika mji huo, kwa ufupi linaeleza hali halisi ya mji huo”.

Akaongeza kuwa: “Kutolewa chapisho hili, jarida linakuwa limeongeza idadi katika matoleo yake kumi na saba ya zamani, jarida hili ni moja ya machapisho muhimu na endelevu yanayo pewa kipaombele na kituo”.

Kuangalia matoleo ya majarida yote yanayo chapishwa na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu fungua toghuti ifuatayo: http://mk.iq/hellah/
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: