Chuo kikuu Al-Ameed: kinaendesha mafunzo yanayo husu namna ya kupambana na changamoto za kazi

Maoni katika picha
Chuo kikuu Al-Ameed chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinaendesha mafunzo ya kujenga uwezo wa watumishi wa chuo, kuhusu namna ya kupambana na changamoto za chuo na uvivu kazini.

Muwasilishaji wa mada hiyo Dokta Hasanaini Adnani Mussawi amesema: “Tumetoa mafunzo haya kwa ajili ya kuboresha utendaji wa kiofisi, hasa upande wa mapokezi, ukizingatia kuwa ndio picha ya kwanza ya eneo la ofisi husika, kunaulazima wa kuhakikisha inawakilisha picha ya ofisi”.

Akaongeza kuwa: “Lengo la mafunzo haya na mengineyo ni kujenga uwezo wa watumishi, na kuwajengea hamasa ya kufanya kazi katika kitengo alichopo”.

Kumbuka kuwa chuo kikuu Al-Ameed kimekuwa mstari wa mbele kujenga uwezo wa watumishi wanaofanya kazi ndani ya taasisi za elimu, kwa lengo la kuhakikisha kinatoa elimu bora kwa wanafunzi katika sekta tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: