Toleo la kitabu cha pili kilicho shinda shindano la uandishi wa kitabu cha Imamu Hussein (a.s) Yara-Nuur

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la kimataifa Rabiu-Shahada imechapisha kitabu cha mshindi wa pili katika shindano la kuandika kitabu kinacho muhusu Imamu Hussein (a.s), lililo fanywa wakati wa kongamano la kimataifa na kitamaduni Rabiu-Shahada awamu ya kumi na tano, kitabu hicho kiliandikwa na Dokta Nuru Saaidiy kiitwacho: (Upekee wa maadhimisho ya Husseiniyya.. utafiti katika turathi za kidini na kijamii).

Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano Sayyid Aqiil Abdulhussein Yaasiriy ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hiki ni kitabu cha pili miongoni mwa vitabu vilivyo shinda, kiliteuliwa na kamati ya majaji baada ya kukamilisha masharti yote ya shindano”.

Akabainisha kuwa: “Kitabu hiki ni tafiti za kielimu zilizo angazia maadhimisho ya Husseiniyya na uhalisia wake kwa kulinganisha na turathi za kidini na kijamii pamoja na nyenzo za kielimu za kisasa”.

Akasisitiza kuwa: “Kitabu hiki kimepasishwa na kamati ya majaji kutokana na umuhimu wake, baaba ya kupitishwa katika orodha ndefu ya vitabu, kitabu hiki ni dirisha linalo onyesha tukio la kudumu la Imamu Hussein (a.s), bila shaka kusambazwa kwake kunafaida kubwa”.

Kwa yeyote anayehitaji kitabu hicho afike kwenye maonyesho ya vitabu ya Atabatu Abbasiyya tukufu, yaliyopo katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: